Author: Bingwa

AGUERO ADAI ANAJIHISI KAMA KAZALIWA UPYA

LONDON, England   STRAIKA wa Manchester City, Sergio Aguero, amesema kwamba anajisikia kama kazaliwa upya, baada ya kupona jeraha la upasuaji wa goti alilofanyiwa mwishoni mwa msimu uliopita. Staa huyo wa timu ya Taifa ya Argentina, alifanyiwa upasuaji huo Aprili mwaka huu na jambo hilo likamfanya azikose mechi sita za mwisho. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 30, ameuanza msimu […]

BEKI INTER AMPONDA RONALDO, AMPA TANO MBAPPE

ROMA, Italia   BEKI wa Inter Milan,  Stefan de Vrij, ni kama amemchokoza straika mpya wa  Juventus, Cristiano Ronaldo, akisema kwamba licha ya kuwa ujio wake utaongeza msisimko katika michuano ya Ligi Kuu ya Italia, Serie A, lakini hana makali kama ya straika wa Paris Saint Germain, Kylian Mbappe. Ronaldo alijiunga na Juve akiwa tayari ameshapata mafanikio na Real Madrid […]

SIMBA WATUA MTWARA; KAGERE, OKWI NDANI

NA WINFRIDA MTOI   KIKOSI cha Simba kimewasili mjini Mtwara jana tayari kwa mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ndanda FC ya huko, unaotarajiwa kupigwa kesho kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona. Simba waliondoka jana asubuhi kwa kutumia usafiri wa ndege, huku kikosi chao kikiwa na wachezaji 20, wakiwamo straika wao hatari, Emmanuel Okwi na Meddie Kagere. Wachezaji […]

PAMBANO LA WATANI … KUZIONA SIMBA, YANGA 7,000/-

DEBORA MBWILO (TUDARCo) NA KELVIN SHANGALI (TUDARCo)   HOMA ya pambano la watani wa jadi, Simba na Yanga, limezidi kupanda baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), jana kutangaza viingilio vya mchezo huo utakaopigwa Septemba 30, mwaka huu, huku cha chini kikiwa shilingi 7,000. Simba ndio watakaokuwa wenyeji wa mchezo huo wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu […]

AMUNIKE ASALIMU AMRI KWA NYONI, MKUDE

NA MWAMVITA MTANDA   KOCHA mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Emmanuel Amunike, amesema atawajumuisha kikosini mwake nyota kadhaa wa Simba, wakiwamo kiungo mkabaji, Jonas Mkude. Mbali ya fundi huyo, wachezaji wengine aliowataja ni beki Erasto Nyoni na mshambuliaji, John Bocco. Mnigeria huyo amefikia uamuzi huo kutokana na kile alichodai kubaini pengo la nyota huyo na wenzake kadhaa wakati […]

LULU DIVA AFUNGUKA KUTENGENEZA NGOZI A.KUSINI

NA ESTHER GEORGE   MREMBO anayefanya vizuri katika Bongo Fleva na wimbo wa Ona, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’, amesema sababu iliyomfanya atengeneze ngozi yake Afrika Kusini ni kuipa hali ya mvuto zaidi. Lulu Diva ameliambia Papaso la Burudani kwamba, anapenda masuala ya urembo na yupo tayari kufanya chochote ili aendelee kuwa mrembo japo hayupo tayari kutaja gharama aliyoitumia kutengeneza ngozi […]

ISHA MASHAUZI ASISITIZA MAADILI KWA WANAWAKE

NA JEREMIA ERNEST   MSANII nyota wa Taarabu nchini, Isha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’, amewataka wanawake kuishi katika maadili na tamaduni  za Kiafrika kwa sababu ni walimu wa watoto katika jamii. Mashauzi anayefanya vizuri na wimbo wa Sudi Sudini, ameliambia Papaso la Burudani kwamba mwanamke ni mwalimu wa mtoto hivyo anapofanya matendo machafu, husababisha madhara kwa jamii. “Watoto wanaishi muda mwingi […]