Author: Bingwa

Azam yazigwaya Simba, Yanga katika usajili

NA SAADA SALIM UONGOZI wa Azam FC, umesema kwa sasa wapo makini katika suala la kufanya usajili wa wachezaji wapya, wakipanga kutoshindana au kugombea mchezaji na klabu nyingine hapa nchini, hasa Simba na Yanga. Azam tayari wameanza kuwaongeza mikataba baadhi ya wachezaji wao, huku wakiendelea kuvutana na mshambuliaji wao, Obrey Chirwa, ambaye bado anasuasua kusaini mkataba mpya kwa madai ya […]

Shungu awapa Simba mchongo DRC

NA MWAMVITA MTANDA SIMBA wamepewa mbinu za kuwawezesha kuifunga TP Mazembe katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa Jumamosi mjini Lubumbashi. Akizungumza na BINGWA jana, Kocha Msaidizi wa AS Vita ya DR Congo, Raoul Shungu, amesema Simba wanatakiwa kujipanga hasa kabla ya kutua Lubumbashi, la sivyo, wanaweza kujikuta wakipoteza mchezo huo. Shungu alisema baada ya TP Mazembe […]

Aussems: Sijawahi kutolewa robo fainali

NA MWAMVITA MTANDA KOCHA Mkuu wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems, amesema kuwa katika historia yake ya kufundisha soka, hajawahi kushindwa baada ya kutinga robo fainali. Aussems, ameyasema hayo alipozungumza na BINGWA jana, ikiwa ni siku chache kabla ya kikosi chake kuivaa TP Mazembe katika mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa jijini Lubumbashi, DR Congo, […]

Simba washtukia mchezo mchafu DRC

ZAITUNI KIBWANA NA HUSSEIN OMAR HOMA ya pambano la robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba na TP Mazembe, imezidi kupamba moto baada ya waamuzi wa mchezo wa marudiano kubadilishwa ghafla na Shirikisho la Soka Afrika (CAF). Simba wakiwa ugenini Lubumbashi, watarudiana na TP Mazembe Jumamosi kwenye Uwanja wa Stade TP Mazembe. Ikumbukwe Simba ililazimishwa suluhu na […]

Serengeti Boys wapo tayari kuanza safari ya Brazil 

NA ISIJI DOMINIC MAWAZO ya timu ya soka ya Tanzania kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 maarufu Serengeti Boys, yameelekezwa nchini Brazil ambapo michuano ya Kombe la Dunia itafanyika baadaye mwaka huu. Lakini ili kufuzu kwa Kombe la Dunia kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys watahitajika kupambana na kutinga hatua ya nusu fainali Kombe […]

SIMBA 0-0 TP MAZEMBE…Pengine Simba wanahitaji kutuonyesha maajabu ya Manchester United, Ajax

NA AYOUB HINJO REKODI ya Simba kushinda michezo yote kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ilishindwa kuendelea baada ya kulazimishwa sare ya kutofungana na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Kwa kiasi kikubwa mashabiki wa Simba waliingia uwanjani wakiwa na uhakika wa kushinda mchezo huo, kwani tayari timu yao ilifanikiwa dhidi ya Mbabane Swallows (eSwatini), Nkana […]

Wameng’ara lakini ubingwa wa ligi wanausikia bombani

LONDON, England RAHA ya soka ni pale unaposhinda mechi na kutwaa ubingwa, lakini jambo hilo mara nyingi huwa si kazi rahisi kutokana na kwamba, mwisho wa siku ni timu moja tu ambayo inaweza kutwaa ubingwa wa mashindano yoyote na ya ligi. Kutokana na jambo hilo kuna baadhi ya wachezaji nyota katika historia ya soka ambao wameshawahi kutwaa mataji makubwa wakiwa […]

TUPA KULE Wakali hawa hawatii mguu Afcon 2019

CAIRO, Misri BAADA ya mechi za kufuzu ambazo zilichezwa kwa mfumo wa makundi, timu 24 zimeshakata tiketi kushiriki fainali za Mataifa Afrika za mwaka huu (Afcon 2019) ambazo zitaanza Juni 29 hadi Julai 19, mwaka huu huko Misri. Hata hivyo, wakati mashabiki wa kandanda barani Afrika wakisubiri kwa hamu kuanza kwa mashindano hayo, yapo mataifa makubwa yaliyoshindwa kupenya, hivyo kukosekana […]

KIBADENI: YANGA SC MASHUJAA

NA ZAINAB IDDY KOCHA na mchezaji wa zamani wa Simba, Abdallah ‘King’ Kibadeni, ameipa tano klabu ya Yanga kutokana na kitendo cha kujitokeza hadharani kuomba msaada wa kifedha kwa wanachama na mashabiki wao, akikiita ni cha kishujaa. Akizungumza na BINGWA jana, Kibadeni alisema viongozi wa Yanga wamefanya jambo kubwa na la kihistoria na linaweza kuwapa matunda mazuri na kuwa somo […]

Tshabalala alia na Yanga, kisa TP Mazembe

NA WINFRIDA MTOI BEKI wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, amesikitishwa na kitendo cha baadhi ya Watanzania, wakiwamo wanaodaiwa mashabiki wa Yanga, kukosa uzalendo na kuishangilia TP Mazembe walipovaana nayo juzi katika mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Simba walilazimishwa suluhu huku timu hizo zikitarajiwa kurudiana […]