Author: Bingwa

MAJEMBE…. Vifaa hivi lazima vimfuate Zidane Madrid

MADRID, Hispania  IKIWA ni takribani miezi tisa tangu aondoke katika klabu ya Real Madrid, hatimaye juzi Kocha Zinedine Zidane, amerejea bila kutarajiwa na klabu hiyo ilithibitisha jambo hilo kupitia katika tovuti yake. Katika kipindi  cha kwanza Zidane  alichokuwa Los Blancos, ilishuhudiwa akifanya makubwa baada ya Mfaransa huyo kuiwezesha kutwaa kwa mara ya tatu mfululizo ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, […]

Lacazette kuivaa Rennes

LONDON, England STRAIKA Alexandre Lacazette leo atakuwamo katika mchezo wa Arsenal dhidi ya  Rennes, baada ya klabu hiyo kukata rufaa ya kufungiwa kucheza mechi hiyo ya Ligi ya Europa na ikakubaliwa na Shirikisho la Soka Ulaya, UEFA. Lacazette alilimwa kadi nyekundu kwa kumpiga kiwiko Aleksandar Filipovic katika mchezo ambao Arsenal waliambulia kipigo cha bao 1-0 wakiwa ugenini dhidi ya BATE […]

Yanga wamgeuka Waziri Mwakyembe

NA HUSSEIN OMAR KLABU ya Yanga imeendelea kuikomalia Serikali ikitaka kusimamia uchaguzi wao wenyewe badala ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kama ilivyoagizwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe. Serikali kupitia Waziri Mwakyembe, iliiagiza uchaguzi wa Yanga kujaza nafasi za viongozi waliojiuzulu kusimamiwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF, kwa kuwa klabu hiyo haina kamati ya […]

SIMBA POWER

Viongozi, wazee, mashabiki waungana kuimaliza AS Vita Sasa Msimbazi nguvu moja, wachezaji washindwe wenyewe NA ZAITUNI KIBWANA KATIKA kuhakikisha wanaibuka na ushindi dhidi ya AS Vita ya DR Congo na kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, viongozi wa Simba, matawi na wanachama wamekutana katika kikao maalumu kujadili ni vipi wanaweza kuwachapa wapinzani wao hao. Simba inavaana na AS […]

Bao lampa Tshishimbi matumaini kubaki Yanga

NA MWAMVITA MTANDA KIUNGO wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi, amesema baada ya kufunga bao la kusawazisha dhidi ya KMC, amepata matumaini ya kuendelea kubaki ndani ya kikosi hicho. Yanga walifanikiwa kuitandika KMC mabao 2-1, katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Tangu kuanza kwa ligi hiyo msimu huu, Tshishimbi, hajafanikiwa kufunga […]

Ndayiragije ataja sababu za Kaseja kutokea benchi

MWAMVITA MTANDA NA TIMA SIKILO KOCHA mkuu wa timu ya KMC, Mrundi Etienne Ndayiragije, amesema sababu ya mlinda mlango namba moja wa timu hiyo, Juma Kaseja, kutokea benchi ni pamoja na kumpa nafasi Jonathan Nahima ambaye bado ni chipukizi. Katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, dhidi ya Yanga, kipa huyo mkongwe alitokea benchi hali iliyoshangaza mashabiki wa soka wakiamini […]