Author: Bingwa

TATIZO SI NAFASI YA MWISHO, ANAJUA ALIPOKOSA?

HAKUNA binadamu asiyewahi kukosea. Kukosea ni suala ambalo lipo tu! Kila binadamu bila kujali hadhi yake wala umri, hukosea. Japo pia kunakukosea kimakusudi ambapo kwa mtu mwenye kujali na kutambua thamani ya kitu au mtu huwa na uwezo wa kuepuka. Kwa kuwa kuna kukosea na hakuna binadamu mwenye uwezo wa kuishi kimalaika, pia inabidi kila mmoja anayekosea asamehewe na kupewa […]

MAMBO YAZIDI KUNOGA BSS

SHINDANO la Bongo Star Search (BSS), linazidi kuchanja mbuga kuelekea kumpata mshindi wa mwaka huu baada ya jana washiriki wengine wawili kutupiwa virago vyao kwenye mashindano hayo. Shindano hilo linaloandaliwa na Kampuni ya Benchmark Production liko katika awamu ya nane mwaka huu likipewa sapoti kubwa ya udhamini wa Salama Condom, kinywaji cha Coca Cola pamoja na kampuni ya ndege ya […]

BASATA YAANDAA KONGAMANO KURUDISHA REGGAE

BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Kampuni ya Reggae Production House iliyo chini ya msanii mkongwe wa reggae, Innocent Nganyagwa, limeandaa kongamano maalumu kwa ajili ya kurudisha hadhi ya muziki wa reggae nchini itakayofanyika leo katika makao makuu ya Basata, Ilala jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo limepangwa kufanyika kwenye ukumbi wa Basata uliopo Ilala Bungoni kuanzia […]

WAKALI WAO WAZIPIGA BAO JAHAZI, MASHAUZI CLASSIC

KUNDI la Wakali Wao linalosimamiwa na Tabit Abdul, limezipiga bao bendi za Jahazi na Mashauzi Classic kwa kumrudisha mwimbaji wao, Asya Mariam ‘Utamu’. Utamu aliyekuwa akiwaniwa na bendi hizo maarufu nchini zenye upinzani mkubwa, ameamua kurejea kwenye bendi yake ya zamani ya wakali wao Akizungumza na gazeti hili, Mariam alisema amerejea rasmi kwenye bendi hiyo baada ya kutofautiana na uongozi […]

KILIFEST YAACHA GUMZO DAR

WASANII mbalimbali mwishoni mwa wiki hii waliacha historia kwenye tamasha la Kilifest lililofanyika kwa mara ya kwanza katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni Dar es Salaam. Tamasha hilo lililoandaliwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, lilikuwa la kuvutia baada ya mchanganyiko wa burudani mbalimbali ikisimamiwa na MaDJ wazoefu kama DJ Summer, DJ Zero na DJ Mafuvu. Mbali na burudani hiyo […]