Author: Bingwa

TUZO YAMTOA POVU RIYAMA

NA JEREMIA ERNEST NYOTA wa filamu nchini, Riyama Ally amesema hakuwa na taarifa za jina lake kuingizwa kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za Sinema Zetu zilizofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam. Riyama Ally ambaye alikuwa kwenye kipengele cha Mwigizaji Bora wa Kike kupitia filamu Mama wa Marehemu, ameliambia Papaso la Burudani kuwa waandaaji wa tuzo […]

LULU ATOA MSAADA AKIWA JELA

NA MEMORISE RICHARD IKIWA ni miezi mine imepita toka mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’, ahukumiwe kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la kumuua msanii Steven Kanumba bila kukusudia, mrembo huyo ametoa msaada wa taulo za kike kwa ajili ya kuwasaidia wasichana, katika kampeni inayoendeshwa na kituo cha runinga EATV. Akizungumza na waandishi wa habari jana maeneno ya Mikocheni Dar es […]

WEMA SEPETU APATA DILI AFRIKA KUSINI

NA KYALAA SEHEYE SIKU chache baada ya kutwaa tuzo mbili katika Tamasha la Kimataifa la Sinema Zetu (SZIFF), Malkia wa kiwanda cha filamu nchini Wema Sepetu, ameingia mkataba na kampuni ya Obuntu Africa yenye maskani yake Afrika Kusini. Wema ameliambia Papaso la Burudani kuwa kampuni hiyo itaisambaza filamu yake ya Heaven Sent katika nchi saba za Afrika hivyo kuendelea kufanikiwa […]

BUFFON: HUYU RONALDO KAMA PELE TU

TURIN, Italia KIPA mkongwe wa Juventus, Gianluigi Buffon, amemfananisha staa Cristiano Ronaldo na Pele. Kauli ya mlinda mlango huyo imekuja baada ya Ronaldo kufungwa mara mbili katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Juve katika mchezo wa juzi wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Katika hali ya kushangaza, uzalendo uliwashinda mashabiki wa Juve na kujikuta wakishangilia bao la […]

RONALDO NYIE, AWEKA REKODI NYINGINE UEFA

TURIN, Italia JUZI, Cristiano Ronaldo alifunga mara mbili na kuiwezesha Real Madrid kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Juventus na staa huyo aliweka rekodi mpya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Mkali huyo mwenye umri wa miaka 33, amekuwa mchezaji wa kwanza kupasia nyavu katika mechi 10 mfululizo za michuano hiyo ya Shirikisho la Soka la Ulaya (Uefa). Aliyekuwa akiishikilia […]

SAKATA LA WAMBURA LAPIGWA DANADANA

NA ZAITUNI KIBWANA MWENYEKITI wa Kamati ya Rufaa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wakili Ebeneza Mshana, amesema hatma ya hukumu ya rufaa ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa shirikisho hilo, Michael Wambura, itajulikana wiki hii. Wambura aliwasilisha rufaa hiyo kupinga adhabu ya kufungiwa maisha kujihusha na soka iliyotolewa na kamati ya maadili ya TFF mwezi uliopita. Awali majibu ya […]

LECHANTRE APATA PIGO SIMBA

NA WINFRIDA MTOI, NJOMBE KOCHA Pierre Lechantre wa Simba ni kama amepata pigo katika kikosi chake, baada ya wachezaji wake watatu kupewa kadi za njano katika mechi ya juzi dhidi ya Njombe Mji, zitakazowafanya kukosa mechi ya Mtibwa Sugar, Aprili 12. Kitendo hicho cha wachezaji hao kupewa kadi, kimemuumiza kocha huyo kwani kinamuharibia mikakati yake ya ubingwa aliyoipanga. Wachezaji waliopewa […]

BOCCO: YANGA IJIANDAE KISAIKOLOJIA

NA WINFRIDA MTOI, NJOMBE BAADA ya mshambuliaji John Bocco kuisaidia Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Njombe Mji kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa juzi, ametangaza hali ya hatari kwa wapinzani wao wakiwamo Yanga. Bocco alipachika mabao mawili katika mchezo huo wa Ligi Kuu uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe […]

PSG NOMA, WAMALIZANA NA FABIHNO

PARIS, Ufaransa MTANGAZAJI wa kituo cha televisheni cha Canal +, Olivier Tallaron, amefichua kuwa kiungo wa Monaco raia wa Brazil, Fabinho, anakaribia kutua PSG. Fabinho mwenye umri wa miaka 24, alikuwa na mchango mkubwa kwa Monaco msimu uliopita, akiipa taji la Ligi Kuu ‘Ligue 1’. Timu hiyo yenye maskani yake jijini Paris, iliishia robo fainali baada ya kung’olewa na Real […]