Author: Bingwa

KWANINI WAMBURA ANAJIONA ANAONEWA?

NA ONESMO KAPINGA WIKI iliyopita Kamati ya Rufani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), chini ya Mwenyekiti wake, Ebenezer Mshana, ilitupilia mbali rufaa  ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho hilo, Michael Wambura. Wambura alikata rufaa kupinga kufungiwa maisha kutojihusisha na masuala ya soka  na Kamati ya Maadili ya TFF, baada ya kubainika  kufanya makosa matatu. Makosa yaliyomtia hatiani Wambura […]

AZAM YABANWA MBAVU SOKOINE

NA SAADA SALIM, Mbeya TIMU ya soka ya Azam FC jana ilishindwa kutamba ugenini baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na wenyeji Mbeya City, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya. Matokeo hayo yameiwezesha Azam kufikisha pointi 45 na kuendelea kubaki nafasi ya      tatu kwenye msimamo wa ligi nyuma ya vinara Simba na […]

MTANZANIA ACHEMKA RIADHA MADOLA

NA GLORY MLAY BAADA ya timu ya ngumi kuondolewa katika michezo ya Jumuiya ya Madola, Mtanzania, Ali Gulam Khamis, ameshindwa kufurukuta mbio za mita 100 zilizofanyika jana. Michezo iliyoanza Aprili 4 mwaka huu, nchini Australia, Gulam alishika nafasi ya nne katika kundi la saba ‘Heat 7’ akitumia sekunde 10.76, matokeo yeye    alishika nafasi ya     44 kati ya wanariadha 65 walioshiriki […]

MAJIMAJI HALI TETE, KOCHA ASALIMU AMRI

NA WINFRIDA MTOI BAADA ya kupoteza mchezo wa 23 dhidi ya Mwadui FC, kocha msaidizi wa kikosi cha Majimaji, Habib Kondo, amesema hali ni mbaya katika kujinasua kushuka daraja msimu huu. Majimaji iliendelea kujiweka katika mazingira mabaya zaidi ya kushuka daraja, baada ya kufungwa mabao 3-2 na Mwadui kwenye dimba la Mwadui Complex, mkoani Shinyanga juzi. Akizungumza na BINGWA jana […]

MOURINHO AWABEZA MAN CITY KWA UBINGWA

LONDON,   England KWA kile ambacho unaweza kusema  ni kama amewabeza, Kocha  Jose Mourinho amewatumia salamu za kuwapongeza  Manchester City  kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England, licha ya kuwatibulia sherehe zao walizoziandaa  katika Uwanja wa  Etihad. Kabla ya mchezo huo wa juzi, baadhi ya mashabiki wa timu hiyo walikuwa wameshajiandaa kushangilia ubingwa kutokana na kuwa walikuwa na uhakika wa kuondoka […]

KILIWAKA ARSENAL WANOGA, JIJI LA MADRID LAKOSA MBABE

LONDON, England STRAIKA Danny Welbeck jana alikuwa mwiba mkali kwa mabeki wa Southampton, baada ya kuziona nyavu zao mara mbili na kuisaidia Arsenal kushinda mabao 3-2. Huku ukiwa ni ushindi wa sita mfululizo katika michuano mbalimbali, matokeo hayo yamewafanya Gunners wafikishe pointi 54, wakihitaji 13 sasa kuwafikia Tottenham wanaoikamilisha ‘top four’. Kikosi cha kwanza cha Arsene Wenger kilikuwa na mabadiliko […]

KATWILA: MTIBWA HATUNUNULIKI

NA MARTIN MAZUGWA        BAADA ya kuandamwa mno na mashabiki wa timu hiyo kutokana na matokeo yasiyoridhisha na kuzushiwa hisia kuwa huwa wanauza mechi, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila, amesema kuwa wamechoshwa na shutuma hizo hivyo kwa sasa ni vipigo tu kwa kila timu watakayokutana nayo, ikiwamo Simba. Mtibwa Sugar inatarajiwa kuikaribisha Simba kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro leo […]

HABARI NJEMA MSIMBAZI

>>Mashabiki waalikwa Moro kumbeba juu juu Bocco leo NA TIMA SIKILO MASHABIKI wa Simba wamepewa habari njema kuelekea mchezo wao wa leo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar, utakaopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, wakitakiwa kutokuwa na wasiwasi kwani ushindi ni lazima. Simba ambao ni vinara wa ligi hiyo wakiwa na pointi 49 baada ya kushuka dimbani […]

YANGA SC NYODO TUPU

>>Ushindi wa juzi wawapa kiburi mjini, wawabeza Simba >>Watamba Chirwa, Yondani, Tshishimbi kumaliza kazi Ethiopia NA WAANDISHI WETU USHINDI wa mabao 2-0 walioupata Yanga katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Welayta Dicha ya Ethiopia juzi, umewapa jeuri wapenzi wa timu hiyo mbele ya watani wao wa jadi, Simba. Kutokana na kipigo […]