AUBAMEYANG AVUNJA REKODI NYINGINE ARSENAL

LONDON, England

STRAIKA, Pierre-Emerick Aubameyang, ameendeleza balaa lake la kuvunja rekodi tangu ajiunge na Arsenal majira ya baridi yaliyopita.

Staa huyo alivunja rekodi hiyo nyingine juzi baada ya kufunga bao katika mchezo wa Ligi Kuu England, ambao waliibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Southampton.

Kabla ya kuweka rekodi hiyo ya juzi, mwishoni mwa wiki iliyopita, Aubameyang, alikuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya Arsenal  kufunga mabao matano katika michezo yake mitano ya kwanza ya Ligi Kuu wakati alipofunga mawili dhidi ya Stoke City.

Kutokana na bao hilo dhidi ya Southampton na ‘asisti’ moja, linamfanya Aubameyang kuwa mchezaji aliyeshiriki kupatikana mabao saba katika michezo yake saba ya kwanza tangu ajiunge na klabu hiyo.

Katika mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Emirates, bao la kuongoza lililofungwa na staa, Shane Long, dakika ya 17 na la kusawazisha lililowekwa kimiani na Charlie Austin dakika ya 73, yalionekana yangewavunja nguvu Arsenal.

Inaendelea………….. Jipatie nakala ya Gazeti la #BINGWA

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*