googleAds

Atalanta yaweka rekodi Ulaya

MILAN, Italia

KLABU ya Atalanta imeweka rekodi ya kufuzu hatua ya 16 bora Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuifunga Shakhtar Donetsk mabao 3-0 usiku wa kuamkia jana. 

Huu ni msimu wao wa kwanza kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya na timu hiyo ya Italia ambayo haikuwa na pointi baada ya michezo minne, wanaungana na Manchester City kutoka Kundi C. 

Kufuzu hatua ya 16 bora kwa Atalanta inatokana Dinamo Zagreb kushindwa kuwafunga mabingwa wa England wakikubali kichapo cha mabao 4-1 nchini Croatia.

Mabao ya Atalanta yaliyopatikana kipindi cha pili yalifungwa na Timothy Castagne, Mario Pasalic na Robin Gosens.

Atalanta walianza kampeni yai kwa kufungwa michezo mitatu mfululizo kabla ya kulazimisha sare dhidi ya Man City ambayo ilibadilisha upepo na kuwarudisha kwenye michuano.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*