googleAds

Arsenal yapata pigo

LONDON, England 

TIMU ya Arsenal itakuwa bila ya huduma ya beki wao tegemeo, Kieran Tierney, aliyeumia bega wiki iliyopita.

Tiernery aliumia wakati Arsenal ilipokuwa ikimenyana na West Ham mchezo wa Ligi Kuu England ambayo walishinda mabao 3-1.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 22, alishindwa kuendelea na mtanange huo na kulazimika kutolewa nje ya dimba.

Hata hivyo, hakuna taarifa yoyote ambayo iliyotajwa ya beki huyo atakuwa nje kwa muda gani.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*