ARGENTINA WAFURAHIA MESSI KUTUPWA NJE UEFA

BUENO AIRES, Argentina

BAADHI ya mashabiki nchini Argentina, wameelezea  furaha yao kuona straika wao, Lionel Messi na timu yake ya Barcelona wakitupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kwa kile wanachodai atapata muda wa kupumzika kabla ya kuanza michuano ya fainali za Kombe la Dunia.

Taarifa kutoka nchini humo zinaeleza kwamba mashabiki hao walizipokea taarifa hizo kwa furaha juzi, baadaya timu hiyo ya Hispania kutupwa nje ya michuano hiyo na AS Roma.

“Kuondolewa kwa Barcelona katika michuano ya Ligi ya Mabingwa ni taarifa njema kwa  Waargentina  kwani, Leo Messi atakwenda katika fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi akiwa hacheza mechi tatu zilizobaki,”uliandika mtandao wa  Ole ukiwakariri baadhi ya mashabiki hao na kufuatia kichwa cha habari kingine kikieleza kuwa : “Ni taarifa njema kwa  Seleccion”.

Inaelezwa kwamba sababu za mashabiki hao kufurahi ni kutokana na kwamba vinara hao kwa sasa wanakabiliwa na michuano ya  La Liga, vilevile kuna mechi ya fainali ya Kombe la  Copa del Rey ambayo itapigwa April 21  mwaka huu ambazo ni mechi kubwa kwa  Messi na huku ikiwapo mechi nyingine  ya  ‘El Clasico’ ambayo itapigwa Mei 6 mwaka huu.

Wakati  Argentina mechi yao ya kwanza itakuwa ni Juni  16 mwaka huu dhidi ya Iceland,ina maana kwamba staa huyo atakuwa na zaidi ya mwezi mmoja wa kupumzika na kutokana na mechi ya mwisho ya ligi kwa  Barca itakuwa ni dhidi ya  Real Sociedad  ambayo itapigwa Mei 19 na huenda Messi hasicheze.

Furaha hiyo ya Waargentina sio kwa Messi tu ni kwa wachezaji wengine,  Nicolas Otamendi na  Sergio Aguero ambao majuzi ilishuhudiwa ndoto zaoa za kubeba taji hilo la Ligi ya Mabingwa Ulaya wakiwa Manchester City zikitoweka baada ya kufungwa na Liverpool na hivyo nao wanatarajiwa kutoa mchango mkubwa kwa  La Albiceleste katika fainali hizo


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*