googleAds

Andy Ruiz apata kisingizio

RIYADH, Saudi Arabia

BONDIA wa uzito wa juu, Andy Ruiz Jr, amekiri kufanya makosa katika pambano la marudiano dhidi ya mpinzani wake, Anthony Joshua ‘AJ’, usiku wa kuamkia jana.

Andy Ruiz aliiweka wazi sababu iliyompelekea kushindwa mpambano huo kwa pointi na kupoteza mikanda mitatu alizokuwa nazo.

“Ulikuwa usiku wa AJ, nadhani sikujiandaa vizuri kwenye mpambano huo, nimeongezeka uzito sana, endapo tutarudiana nitahakikisha niko kwenye shepu nzuri,” alisema bondi huyo raia wa Mexico.

Mkali huyo alikuwa na uzito wa pauni 283 mwezi Juni mwaka huu kabla ya kushuka ulingoni kutwangana na AJ kwenye pambano hilo la marudiano la uzito wa juu.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*