Anayedaiwa kumuua Nipsey Hussle akamatwa

LOS ANGELES, MAREKANI

MTUHUMIWA namba moja wa mauaji ya Nipsey Hussle, Eric Holder, ametiwa nguvuni na idara ya polisi mjini Los Angeles, Marekani, akituhumiwa kummiminia risasi zaidi ya tano rapa huyo Machi 31, mwaka huu.

Eric Holder ambaye ni miongoni mwa vijana wanaotokea kwenye vikundi vya kihalifu Los Angeles, alitiwa nguvuni saa chache baada ya polisi kuachia ‘footage’ za cctv zikimwonyesha Holder akifanya tukio hilo nje ya duka la nguo la Nipsey.

Taarifa zinadai kwamba, muda mchache baada ya idara ya polisi kutangaza Eric Holder kuhusika na mauaji hayo, ndugu zake wawili waliuawa huku ikiaminika kundi rafiki na Nipsey limeanza kulipa kisasi baada ya kifo cha rafiki yao.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*