Amri Said: Pointi tisa tu zinatosha kubaki TPL

ZAITUNI KIBWANA

KOCHA Mkuu wa Biashara United, Amri Said, amesema anasaka pointi 12 ikishindikana apate tisa ili kuibakisha timu yake Ligi Kuu Tanzania Bara.

Biashara United imebakisha mechi nne pekee kabla ya kumalizika kwa Ligi Kuu Tanzania Bara, ikishika nafasi ya 18 kati ya mechi 35 ilizocheza, ikikusanya alama 40 pekee.

Akizungumza na BINGWA jana, Amri Said, alisema ikishindikana kupata pointi 12, walau aambulie pointi tisa ili ajihakikishie kusalia kwenye michuano hiyo msimu ujao.

“Tutasalia Ligi Kuu Tanzania Bara, tukifanikiwa kupata pointi 12 tu au walau tisa basi tutakuwa na uhakika wa kuendelea kuwamo msimu ujao,” alisema.

Alisema ili kuhakikisha anazoa pointi hizo, kamwe hatotaka mzaha na wachezaji na kila mmoja atapaswa kujituma kwa hali na mali ili kutimiza malengo. “Malengo ni makubwa, mechi zimebaki chache sitataka mzaha na mchezaji yeyote, ili kuhakikisha tunasalia kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara,” alisema


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*