AMNESTY WAIUMBUA QATAR MAANDALIZI KOMBE LA DUNIA

LONDON, England


 

SHIRIKA lisilokuwa la kiserikali la kutetea Haki za Binadamu, Amnesty International, limesema wajenzi wengi wanaojenga uwanja wa fainali ya Kombe la Dunia nchini Qatar, wanafanya kazi kwenye mazingira magumu, wakiteswa zaidi na njaa.

Ripoti hiyo ya Amnesty ilisema kuwa takribani wafanyakazi 78 kutoka mataifa ya India, Nepal na Ufilipino, wanapata shida mno katika kibarua chao hicho, kwani hawana hela zinazoweza kuwasaidia kupata chakula.

Inaeleweka kwamba, waajiriwa katika kibarua hicho wamefanya kazi hiyo kwa miezi kadhaa sasa bila kupata malipo yao na baadhi wanadai hadi pauni 4,000 (Sh milioni 11.9).

Mradi wa matengenezo hayo ambao utagusa zaidi mji wa Lusail, unategemewa kugharimu kiasi cha pauni bilioni 34 (Sh trilioni 101), lakini matengenezo ya uwanja mpya utakaochukua watu 80,000 ndio utakaochukua nafasi kubwa.

Hata hivyo, mkandarasi anayeshughulikia zoezi hilo, Kampuni ya Mercury MENA, walisema kwamba, wanakabiliwa na matatizo ya mzunguko wa fedha na waliwaeleza wazi Amnesty kuwa hawana uwezo wa kuwalipa wafanyakazi hao.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*