googleAds

Ameacha rekodi zipi?

*KOBE amestaafu akiwa anashika nafasi ya nne katika orodha ya wachezaji waliofunga pointi nyingi NBA (33,643), zote akifunga akiwa na Lakers.

*MSHINDI mara mbili wa medali ya dhahabu katika michuano ya Olimpiki, akifanya hivyo akiwa na timu ya taifa ya Marekani (2008 na 2012).

*MCHEZAJI mwenye umri mdogo zaidi kufikisha pointi 30,000 katika historia ya NBA. Kobe aliweka rekodi hiyo akiwa na miaka 34.

*MCHEZAJI pekee wa kikapu kuinyakua tuzo ya Oscar, ambayo hutolewa katika tasnia ya filamu. Kobe aliiweka mkononi kupitia filamu yake ya dakika tano aliyoachia mwaka 2015, ambayo alielezea mapenzi yake kwa mchezo wa kikapu.

* HADI anatundika daluga, alikuwa ameibeba mara mbili tuzo ya Mchezaji Bora wa Msimu, wapenzi wa kikapu wakiifahamu kwa jina la MVP. Alifanya hivyo msimu wa 2008-09, kisha akaitetea 2009-10.

* AKIWA ameshuka dimbani mara 16, Kobe anabaki kuwa mchezaji aliyecheza mechi nyingi Sikukuu ya Krismasi katika historia ya NBA.

*ANASHIKA nafasi ya pili kwa wachezaji waliofunga pointi nyingi (81) katika mchezo mmoja, akizidiwa na Wilt Chamberlain (100) aliyefanya hivyo mwaka 1962.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*