Ally Kisaka kurithi mikoba ya Kocha Sumbu, Pamba SC ya Mwanza

Damian Masyenene, Mwanza

Baada ya aliyekuwa kocha wa timu ya soka ya Pamba SC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL), Juma Yusuph Sumbu kuachana na timu hiyo kutokana na maradhi ya moyo na kupooza timu hiyo sasa imepata kocha mpya, Ally Kisaka atakayeinoa hadi mwisho mwa msimu.

Kabla ya kocha Kisaka timu hiyo ilikuwa chini ya Kocha Msaidizi, Yangoo Mamboleo aliyeiongoza katika mechi mbili za FDL dhidi ya Boma na nyingine dhidi ya Green Worriors.

Kabla ya kurudi Zanzibar kwa matibabu Sumbu amekuwa kocha wa Pamba kuazia Septemba mwaka jana akitokea timu ya Chuoni ya Unguja, Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya Habari na Msemaji wa Klabu hiyo, Johnson James, kocha huyo ana leseni C ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), ataiongoza timu hiyo kwenye mechi ya Rhino Rangers ya Tabora.

“Tumeingia makubaliano na Kisaka kutokana na aliyekuwa kocha wetu kuugua ghafla na kushindwa kuendelea na majukumu yake, kwa mujibu wa kanuni ya 72 ya ligi daraja la kwanza Kocha wetu Msaidizi, Yangoo Mamboleo alitakiwa kuiongoza Pamba kwa michezo mitatu tu kama kocha msaidizi na mechi hizo zimekwisha ndiyo maana tumemleta kocha Kisaka,” amesema Johnson.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*