Allegri aipa masharti makali Man United

MANCHESTER, England

ALIYEWAHI kuifundisha Juventus, Massimiliano Allegri amewaambia Manchester United kama watamwitaji kuchukua mikoba ya Ole Gunnar Solskjaer yupo tayari lakini inabidi wafanye haraka kumtimua kocha huyo.

Allegri kwa sasa hana kazi tangu alipoachana na Juventus msimu uliopita baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka mitano na kuipa mafanikio ya kutawala soka la nchini Italia.

Kwa sasa, Manchester United wapo nafasi ya 12 katika msimamo wa Ligi Kuu England baada ya kucheza michezo nane, wameshinda miwili, sare tatu na kufungwa mara tatu.

Allegri mwenye umri wa miaka 52 anafukuzia kwa ukaribu nafasi hiyo, kilisema chanzo kutoka katika kituo cha Gazzetta dello Sport cha nchini Italia. 

Lakini, anachokitaka kocha huyo Manchester United wafanye uamuzi wa haraka kumfukuza Solskjaer ambaye alisaini mkataba wa miaka mitatu Machi, mwaka huu. 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*