ALIYEMSHTAKI CHRIS BROWN HOI KITANDANI

LAS VEGAS, Marekani


 

MWANADADA aliyeibua madai ya kubakwa katika mjengo wa staa, Chris Brown, Liziane Gutierrez, ameripotiwa kuwa katika hali mbaya ya kiafya.

Mwaka jana, mlimbwende huyo alifika mahakamani kumfungulia mashtaka Chris, akisema alishirikiana na wenzake kumbaka katika moja ya vyumba vya hoteli iliyopo mjini Las Vegas.

Inaelezwa kuwa kesi hiyo ilimwezesha kukinga kitita cha Dola za Marekani 70,000 (zaidi ya Sh mil 150 za Tanzania).

Liziane mwenye umri wa miaka 32, ametajwa kudhurika vibaya na upasuaji aliokuwa akifanya kuurekebisha mwili wake uwe wa kuvutia.

Mrembo huyo raia wa Uturuki, amekuwa sehemu ya mijadala ya mitandaoni tangu alipojitokeza kusema alifanyiwa uhuni na Chris mwaka jana.

Mercy Johnson kuacha uigizaji kisa siasa?


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*