ALAMA ZA MWANAMKE ANAYEKUHITAJI KIMAPENZI

NA RAMADHANI MASENGA


KARIBU kila kitu huwa na dalili zake. Mvua ina dalili, homa ina dalili, hata kwa mujibu wa mafundisho ya dini siku ya mwisho pia ina dalili zake. Kupitia hizo dalili, ndiyo hasa huwa tunajua uwepo au kutokuwapo kwa kitu.

Japo si mara zote mawingu yakitanda huwa mvua inanyesha, ila huwa mara nyingi yakitanda mvua hunyesha. Kilichokusudiwa hapa ni kwamba, kuna mienendo na mambo hutokea kutoa ufahamu wa kitu fulani.

Wanawake ni tofauti sana na wanaume. Matendo mengi yanayofanywa na wanaume ni wanawake wachache sana huweza kufanya, tena pengine hufanya chini ya viwango na mbinu husika zinazotumiwa na wanaume.

Yapo matendo mengi kama kukimbia, kupigana, hata jinsi wanavyowaza na kuamua. Ila hapa najadili kuhusu mapenzi.

Si mara zote mwanamke huwa anamwambia mwanamume hisia zake moja kwa moja, kama ambavyo wanaume wamekuwa wakifanya. Ndiyo kuna wanawake wana uwezo huo, ila ni wangapi? Ni wachache sana.

Katika jamii jukumu la kueleza hisia za mapenzi linaonekana hasa ni la kiume. Wanawake wamebaki kuwa wasikilizaji tu au kama akiwa naye kapenda kweli hubaki kuonesha hali hiyo kupitia ishara.

Wanawake wengi hufanya hivi badala ya kusema nini wanajihisi kwa kina fulani. Unamjua mwanamke anayekupenda wewe? Hata kama hajasema akiwa na ishara zifuatazao huyo atakuwa na hali ya hisia fulani za upendo na wewe.

(i)Atapenda kuongea na wewe, kila anapopata nafasi atapenda kuwa na wewe karibu mkiongea. Atakuwa makini na kufanya kila analoweza kuona kuwa anaheshimu mazungumzo yako na uwepo wako. Inaweza kuwa huwa anaongea na watu wengi, ila uongeaji wake utakuwa tofauti sana na akiwa na wewe. Kwako atakuwa na heshima zaidi na utulivu zaidi, tena akiwa ana ujasiri wakati mwingine atapenda kugusana na wewe muwapo katika mazungumzo yenu. Hata kama hakuna ulazima anaweza kugusisha bega lake kwako au hata kugongesha viganya. Yote anafanya katika hali ya kuipa furaha nafsi yake pamoja na kuonesha ni kwa namna gani kwako alivyo huru.

Mwanamke huwa muoga sana kugusana na mwanamume, ila woga huo hutoweka akiwa na hisia fulani nzuri juu yako. Hata kama ukimgusa bahati mbaya maeneo kama ya maziwa na hata kwenye makalio hawezi kukutukana wala kujisikia vibaya kama akifanyiwa na mtu asiye na hisia naye.

(ii)  Atakuwa na nidhamu kwako, ndiyo, anaweza kuwa mtu wa nidhamu siku zote. Ila hapa kwako itakuwa zaidi.

kwa kipindi chote anachokutana na wewe atahakikisha anaonesha hali ya nidhamu kwako na unyenyekevu. Kwake hali hii itakuwa na tafsiri mbili; kwanza anataka kuonesha kwamba wewe ni mtu muhimu sana kwake ila pili atataka uone raha na furaha kuongea na yeye.

Wakati mwingine nidhamu yake huwa kama pia imechangiwa na aina fulani ya woga, ila hufanya hivi katika namna ile ile ya kukuonesha ubora na hadhi katika moyo wako.

(iii) Atafanya kitu kwa ajili yako, hata mkiwa mmekutana pamoja halafu wewe ukaonesha una shida na kitu fulani, aidha nguo au hata kitabu, yeye kama pesa anayo atataka kukununulia.

Jambo hili kwake huwa ni katika hali ya kuweka alama katika maisha yako na kuonesha ni kwa kiasi gani ulivyo na umuhimu katika maisha yake. Hata nauli mkiwa pamoja atataka kukulipia ikiwa tu ana pesa za kutosha.

Atajitahidi kwa kila hali kukuonesha yuko tayari kwa ajili ya kukupa furaha na kuonesha umuhimu wako katika maisha yake.

(iv)  Kukupa zawadi, haijalishi ni ya gharama kiasi gani, ila atataka kukupa zawadi ikipatikana nafasi ya kufanya hivyo.

Zawadi ni kipimo cha thamani na kumkumbuka mtu. Yeye atafanya hivi katika hali hiyo na ili umfikirie zaidi. Tena akiwa mjanja zaidi anaweza kukupa zawadi zenye uashiriao wa mapenzi na kumbukumbu.

Kwa mfano anaweza kukununulia saa au kitu chenye maandishi yenye kujenga hali ya mapenzi na kuonesha dhamira yake kwako. Hapa wengi huwa ni waoga kutoa zawadi za maua au kadi, japo kuna wengine wana uwezo wa kufanya hivyo.

Woga wao unakuja kutokana na zawadi husika kuwa wazi sana kuonesha dhamira zao.

(v)  Kutaka kujua mengi kuhusiana na familia yako, ili kuonesha ni kwa namna gani anahitaji nafasi katika maisha yako, atataka kujua mambo unayoyapenda na kujua vitu muhimu katika familia yako.

Atataka kujua wewe ni wa ngapi kuzaliwa, kabila lako na asili yako kwa ujumla. Pia atataka kujua chakula na mavazi unayopenda, aina ya familia na mwanamke unayetaka kuwa naye katika maisha yako.

Kwa mwanamke mjanja yeye atakubana sana katika maswali ya namna hii, ila nawe ukitaka kumpa maswali atakujibu kwa namna ya majibu yako kwake yalivyo.

Kwa mfano; unaweza kusema unapenda mwanamke wa aina Fulani, ila kama yeye tayari kakuuuliza na umemjibu swali la mwanamke unayempenda atakujibu kwa mujibu wa jibu  lako. Hata kama ataongeza kitu ila si katika namna ya kutoa maana halisi ya kitu ulichoongea.

(vi)  Atata kuishi kwa namna unavyopenda, baada ya kujua wewe ni mtu wa aina gani kupitia maswali na mfumo mzima wa maisha yako, atataka kuishi namna unavyopenda ili uweze kuvutiwa naye. Kama atajua hupendi mwanamke mapepe hata siku moja hawezi kujichetua kwa kuamini kwa kufanya hivyo atakuwa anakufukuza.

Akijua hupendi mwanamke mwenye marafiki wengi wa kiume hata kama alikuwa nao atafanya kila njia kuachana nao. Yote atayafanya katika hali na namna ya kukuonesha kuwa yeye ni mtu anayekufaa katika maisha yako.

(vii)   Atakuwa na huruma zaidi kwako, akihisi una matatizo au unapitia katika hali ngumu ya kimawazo atataka kuwa karibu zaidi na wewe pamoja na kukupa maneno ya kukutia nguvu na imani zaidi. Hata siku moja hawezi kukuacha ukiwa unataabika kifikra na kuumia peke yako, katika kila namna atakayoweza atataka kuonesha ni kwa kiwango gani anaweza kukufuta machozi na kujenga tena tabasamu katika sura yako.

(viii)  Atazungumzia mipango yake ya mbele kwako, ili kukuvuta zaidi kwake ataweza kukueleza nini mipango yake ya baadaye na namna gani alivyo na dhamira ya kweli katika kufikia ndoto zake.

Atafanya hivyo kukufanya ujue yeye ni mtu mwafaka na bora sana katika maisha yako. Atataka ujue unapoingia naye katika uhusiano basi, utakuwa na mtu mwafaka katika maisha yako ambaye atakufanya uyaone maisha mepesi kwa usaidizi wake.

(ix)  Atakusikiliza kwa makini na kutekeleza unayopenda, kwa ajili ya kukuvuta kwake atakuwa makini katika kukusikiliza na kufanya yale unayopenda kufanyiwa au unayotamani kufanyiwa.

Hata bila kumtaka afanye yeye atafanya kwa umakini huku akiwa makini kuona mwitikio wako katika suala husika, akiona umefurahia atafanya hivyo kadri atakavyopata wasaa wa kufanya.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*