Aiyee azituliza KMC, Lipuli, Polisi Tanzania

NA TIMA SIKILO

MSHAMBULIAJI wa Mwadui, Salim Aiyee, amezitaka klabu zinazohitaji saini yake kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kumpa muda wa wiki moja ili aweze kutoa uamuzi sahihi.

Aiyee ambaye aliifungia Mwadui mabao 18 msimu wa ligi iliyomalizika hivi karibuni, anawindwa na klabu mbalimbali, zikiwamo KMC, Polisi Tanzania na Lipuli.

Akizungumza na BINGWA jana, Aiyee alisema kwa sasa ni mchezaji huru, baada ya kumaliza mkataba wa kuitumia Mwadui, hivyo anaweza kufanya mazungumzo na klabu yoyote.

Aiyee alisema malengo yake ni kucheza timu ambayo itafanya aonekane na klabu mbalimbali ili aweze kupata soko.

“Kuna klabu nyingi, ikiwemo Lipuli, KMC, Tanzania Prisons na Polisi Tanzania zimenipigia simu ila nitajua naenda kucheza wapi baada ya kuonana na familia yangu,” alisema Aiyee.

Aiyee alisema malengo yake kuendelea kuonyesha kiwango bora katika timu atakayosaini mkataba.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*