Aiyee aitolea nje Simba

ZAINAB IDDY

KINARA wa mabao katika kikosi cha Mwadui FC, Salim Aiyee, ameitolea nje Simba baada ya kusema kuwa hawezi kusaini kwa Wekundu wa Msimbazi.

Aiyee aliyeifungia Mwadui FC mabao 16 na kuwa kwenye mbio za ufungaji bora msimu huu, ni miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kuhitajika na kocha Mbelgiji, Patrick Aussems.

Akizungumza na BINGWA jana, Aiyee alisema licha ya kuwepo kwa taarifa za yeye kufanya mazungumzo na Simba, huku wengine wakijaribu kumshawishi ili ajiunge na Wekundu wa Msimbazi lakini yeye bado hajafikiria kufanya hivyo.

“Sijawaza kwenda kucheza Simba msimu ujao kwa kuwa nina mipango mingine inayoweza kukamilika muda si mrefu.

“Si kwamba Simba ni timu mbaya, kila mtu ana malengo aliyojiwekea binafsi kabla sijaamua kwenda kucheza timu kubwa lazima kuna vitu nivikamilishe, hivyo sidhani kama msimu ujao nitakuwa huko ninakotajwa kwenda.”


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*