googleAds

Abraham abaguliwa kisa penalti!

LONDON, England

TAASISI ya kupambana na ubaguzi wa rangi kwenye mchezo wa soka, Kick It Out, imeaani vitendo anavyofanyiwa mshambuliaji wa Chelsea, Tammy Abraham, baada ya kichapo kutoka kwa Liverpool kwenye UEFA Super Cup.

Baadhi ya mashabiki wa Chelsea walimshukia Abraham kwa kitendo chake cha kukosa penalti dhidi ya Liverpool, na kuwazawadia majogoo hao wa Anfield taji kwa ushindi wa penalti 5-4.

Penalti hiyo aliyopiga Abraham, iliokolewa vyema na mlinda mlango wa Liverpool, Adrian San Miguel, na kuwaibua mashabiki kupitia mtandao wa Twitter ambao walianza kumshambulia kinda huyo kwa kauli za kibaguzi.

“Tutakuwa pamoja na Tammy na tuzitaka kampuni za mitandao ya kijamii pamoja na Twitter, kushughulikia watu hawa wanaoendelea na vitendo vya ubaguzi,” ilisema kauli ya Kick It Out.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*