Aachana na demu wake kisa Wizkid

LAGOS, Nigeria

RAPA anayetikisa vilivyo kwenye soko la muziki la Nigeria, Skales, amebwagana na mpenzi wake, huku sababu ya kufikia uamuzi huo ikitajwa kuwa ni msichana huyo kumpenda staa Wizkid.

Baada ya kuachana na mchumba wake huyo, imedaiwa kuwa Skales ameamua kutoka na kidosho mmoja kutoka pande za Ethiopia.

Wizkid na Skales wamekuwa kwenye vita ya maneno tangu mwaka 2015 na sababu kubwa inayotajwa kuwagombanisha ni ngoma ya Super Star’.

Kupitia mitandao ya kijamii, Skales alidai kuwa yeye ndiye aliyemwandikia Wizkid wimbo huo, jambo lililomkasirisha staa huyo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*