50 CENT APANGA KUVURUGA TAMASHA LA JA RULE

NEW YORK, Marekani


 

RAPA mkongwe, 50 Cent, ameamua kulifikisha katika ngazi ya juu bifu lake na nguli mwenzake, Ja Rule, baada ya kununua viti vyote vya mstari wa mbele ili viwe wazi wakati wa tamasha hilo la hasimu wake.

Kwa mujibu wa gazeti la Metro, rapa aliyejizolea umaarufu kupitia albamu yake ya ‘Get Rich or Die Tryin’,  anaonekana kumchokoza staa huyo mwenzake, baada ya kudaia kununua viti 200 ili viwe wazi wakati wa tamasha hilo ambalo limepangwa kufanyika Novemba 9 mwaka huu mjini Arlington Texas.

Kupitia ujumbe huo, staa huyo aliambatanisha pia picha inayoonesha viti vya mbele vikiwa wazi na huku yeye  akiwa amekaa kati kimoja wapo na baadhi ya mashabiki wakiwa kwa mbali nyuma yake.

Mbali na picha hizo, pia kinara huyo aliongeza tena ujumbe mwingine wa kuliponda tamasha hilo akisema kuwa halitakuwa na shamrashamra zozote bali eneo hilo litakuwa kama chumba cha kupumzikia watoto wake.

‘Watu wanafikiri nina maana ya kwenda kushuhudia kitu hicho. Dola 15 zinasubiri kile ninachofanya Ja Rule,” aliandika katika ujumbe wake alioutuma kupitia mtandao wake wa Instagram na huku akiambatanisha na picha za tiketi zinazouzwa kwenye mitandao.

“Nimeshanunua tiketi za viti 200 ambavyo siku hiyo vitakuwa wazi,” aliongeza kupitia ujumbe huo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*