googleAds

Kagere apata mpinzani

NA WINFRIDA MTOI

MSHAMBAULIAJI wa timu ya Polisi Tanzania, Sixtus Sabilo, amesema atakula sahani moja sambamba na Meddie Kagere wa Simba kuhakikisha anaibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Sabilo aliyesajiliwa na Polisi katika msimu huu akitokea klabu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC),  Jumamosi iliyopita alifunga mabao mawili, wakati timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Ushirika, Moshi.

Akizungumza na BINGWA jana, Sabilo, alisema tangu ligi hiyo imeanza, alikuwa hayupo katika kiwango kizuri, hivyo kushindwa kuonesha makali.

Nyota huyo alisema kitendo cha kufunga mabao mawili katika mchezo mmoja, kimempa morali ya kuendelea kujituma mazoezini ili aweze kuwa kati ya wafungaji bora kama ilivyokuwa kipindi anachezea Stand United.

“Kwa muda mrefu nilikuwa nimefunga bao moja tu, sababu nilikuwa sipo katika kiwango changu, lakini sasa najiona kabisa nimechanganya,”alisema Sabilo.

Alisema malengo yake katika mechi zilizobaki ni kufikisha mabao 10 au zaidi ili aweze kwenda sambamba  na wale waliofunga mabao mengi akiwamo Kagere na wengine.

Katika orodha ufungaji, Kagere anaongoza kwa kufikisha mabao 10, akifuatiwa na Paul Nonga aliyefunga mabao nane na Daruesh Saliboka mabao saba wote kutoka Lipuli.

@@@@@@


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*