Mkongwe adai mabosi Arsenal wamemsaliti Emery

LONDON, England

STRAIKA wa zamani wa Arsenal, Charlie Nicholas, amesema kuwa mabosi wa kikosi hicho wameshindwa kumsaidia kocha wao wa sasa, Unai emery, baada ya Arsene Wenger kuondoka.

Charlie alidai kuwa hata kabla ya msimu kuanza, Emery alihitaji wachezaji ila kutokana na bajeti iliyowekwa na timu hakuwa na uhakika wa kupata nyota walio na uwezo mkubwa zaidi.

Mkongwe huyo aliendelea kusema kuwa mabosi wa Arsenal walimdanganya Emery kwa kudai watamsaidia kwa kila kitu atakachohitaji hapo.

“Siwezi kuwa muongo, mabosi wa Arsenal wamemsaliti Emery tangu alipochukua nafasi ya Wenger kikosini, timu inaenda tu lakini kuna mengi yapo ndani.

“Hata wachezaji waliosajiliwa si idadi ile aliyohitaji Emery, ila alikuta bajeti ya timu hairuhusu,” alisema Charlie.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*