JOSE MARA AFUNGUKA KUOA TENA

NA CHRISTOPHER MSEKENA

MWANAMUZIKI wa dansi katika bendi ya Mapacha Watatu, Joseph Michael ‘Jose Mara’, amesema hafikirii kuoa tena baada ya kutengana na mke wake Monica mwaka mmoja uliopita.

Jose Mara alisema yeye ni mtu makini na mwenye kijitathmini anapopitia majaribu, hivyo hafanyi vitu kwa mihemko na mawazo ya watu ndiyo maana anatumia muda huu kutafakari na kumwomba Mungu ampe mwongozo mzuri.

“Nimeachana na aliyekuwa mke wangu, mahusiano yetu bado yapo kwa sababu kutengana si vita hasa mnapokuwa na watoto, kwa hiyo wanaokuwa na chuki wanapoachana ni matokeo ya chuki na kutokuwa na Mungu,” alisema Jose Mara ambaye ni baba wa watoto wawili Michael na Jose Jr.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*