CARRICK: NILITESEKA KWA MIAKA MIWILI

MANCHESTER, England

KIUNGO wa zamani wa Manchester United, Michael Carrick, amesema alikuwa katika mawazo na sintofahamu kwa kipindi cha miaka miwili baada ya kupoteza mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2009 mbele ya Barcelona.

Carrick ambaye hivi sasa ni mmoja ya makocha waliopo katika benchi la ufundi la Manchester United, alibainisha hayo katika kitabu chake kipya alichokizindua hivi karibuni na kujulikana kwa jina la ‘Between the line’.

“Nilipoteza mpira kwa kichwa na Iniesta alikuwa karibu na kumpasia Messi ambaye alirudisha pasi kwa Iniesta haraka sana na kukatisha mbele yangu na Anderson, kisha kumpasia Eto’oo aliyefunga bao la kwanza kwa Barcelona,” aliandika Carrick katika kitabu chake hicho.

Baada ya miaka miwili kupita Manchester United walikutana na Barcelona tena katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na timu hiyo kutoka nchini England, ilipoteza kwa mara nyingine kwa mabao 3-1 ndani ya Uwanja wa Wembley.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*