googleAds

LYON: TULISTAHILI KIPIGO CHA SIMBA

NA WINFRIDA MTOI

Kocha Mkuu wa African Lyon,  Mfaransa Soccoia Lionel, amekiri kuwa kipigo walichopata kutoka kwa Simba kilistahili kutokana na ubora wa  Wekundu hao wa Msimbazi kuanzia kikosi hadi kifedha.

African Lyon juzi ilifungwa na Simba mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam ikiwa ni mchezo wa tatu mfululizo kupoteza katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Lionel alisema Simba ni timu yenye uwezo kuliko wao, kwa sababu  mshahara wa mchezaji mmoja wa Wanamsimbazi hao ni sawa na fedha ya kuhudumia kikosi kizima cha African Lyon.

“Mechi ilikuwa ngumu kwetu,  tusingeweza kushindana na Simba, ukiangalia ni bora kila sehemu hata maisha yao ni tofauti na sisi kwa kuwa  mshahara wa mchezaji wao mmoja  unahudumia timu yetu nzima,” alisema.

Alisema kutokana na hali hiyo, ni ngumu kushindana na kikosi hicho na kutarajia kupata matokeo ya ushindi mbele ya timu iliyosheni wachezaji wenye viwango vikubwa


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*