googleAds

BAJAJI NYINGINE YA SPORTPESA YATUA KIGOMA

NA MWANDISHI WETU

Mkazi wa Kigoma, Hamis Kanuma, amekabidhiwa bajaji yake aliyoshinda kutoka Kampuni ya kubashiri mechi za soka ya SportPesa, hiyo ikiwa ni zawadi ya mshindi wa nne.

Akizungumza wakati wa kumkabidhi bajaji mshindi, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mjini, Samson Nonga, alisema Kanuma alipata ushindi wa bajaji hiyo kutoka SportPesa baada ya kutupia ubashiri kwa Sh 1,000 tu.

“Mcheze SportPesa, mnaona mwenzenu amecheza kwa kiasi kidogo cha pesa (fedha) tu, lakini mwisho wa siku amepata bajaji yenye thamani ya mamilioni, acheni kuzubaa, huu ndio wakati wenu kushtuka maana unaweza kulala masikini, lakini kesho SportPesa ikakufanya uamke na utajiri. Nawaombeni sana wana Kigoma Mjini tusikubali hii itupite,” alisema Nonga.

Aidha, Nonga alisema ushindi huo unaweza kumfanya mtu kuondokana na umasikini kama ambavyo imetokea kwa Kanuma, kwani imani yake ni kuona bajaji hiyo ikiinua kipato cha kijana huyo na kuondokana na dimbwi la umasikini

Kwa upande wake, mshindi huyo wa droo ya nne, alisema aliifahamu SportPesa kupitia mitandao ya kijamii pamoja na kwenye runinga na anaamini kuwa ushindi huo umekuja muda sahihi kwenye maisha yake.

“Nina furaha sana, hakika bajaji hii inaenda kunisaidia na kitu cha kwanza kabisa nitakachofanya kutokana na pesa (fedha) nitakayopata kupitia bajaji hii, nitahakikisha nanunua kiwanja, pili itanisaidia kuikwamua familia yangu maana natokea katika familia ya kimasikini. Lakini tatu naamini itamsaidia mwanangu kusoma na kufaulu vyema kwenye mitihani yake maana hakutakuwa na shida ya ada,” alisema Kanuma.

Mloto Thabiti ambaye ni rafiki mkubwa wa Kanuma, alikuwa shuhuda wa mwenzake huyo wakati akikabidhiwa bajaji mpya kutoka SportPesa, ambapo alisema amejisikia faraja kuona rafiki yake ameshinda.

Bado mchakamchaka wa Shinda Zaidi na SportPesa unaendelea na kila Mtanzania ana nafasi ya kujishindia bajaji, kitendo cha kupiga *150*87# kitakupeleka kujisajili na timu ya ushindi na moja kwa moja unaweka fedha kuanzia 1,000 na kuanza kucheza bila kusahau kucheza mara nyingi ndiyo siri ya kushinda.

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*