googleAds

NINJA APATA UJIKO MECHI YA WATANI

NA TIMA SIKILO

BEKI wa Yanga, Shaibu Abdallah ‘Ninja’, jana alitoka na ujiko Uwanja wa Taifa baada ya kuonyesha kandanda safi na kusaidia kuimarisha safu ya ulinzi ya Yanga.

Kati ya mambo yaliyompa ujiko beki huyo, ni uwezo wake wa kuzuia pasi za viungo wa Simba kwa staili ya kupiga kwanja.

Beki huyo anayeelekea kufuata nyayo za nahodha wa zamani wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, alifanya hivyo zaidi ya mara tano, huku kazi itakayokumbukwa zaidi ni kuzuia kwa nguvu akitumia zaidi guu lake la kulia, akimpa shida Mganda Emmanuel Okwi ndani ya 18 hasa kipindi cha kwanza.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*