NYOTA MAN UNITED WAMKAZIA MOURINHO

MANCHESTER, England


 

IMERIPOTIWA kuwa kuna moto umewaka katika klabu ya Manchester United, kwani baadhi ya nyota wamekasirishwa na tabia ya Jose Mourinho kuwadhalilisha wenzao.

Baada ya kutolewa kwa mikwaju ya penalti na Derby katika michuano ya Kombe la Carabao, Mourinho aliwatupia maneno makali Phil Jones aliyekosa penalti na Eric Bailly.

Alisema hivi: “Nilijua tu kuwa tunakwenda kupata tabu tukiwa na Jones na Eric. Nililijua hilo mapema.”

Kauli hiyo, ambayo ilitanguliwa na nyingine ya Mourinho kumwambia Paul Pogba hatakuwa tena nahodha, imetajwa kuwachefua nyota wengine kikosini.

Hata hivyo, ingawa hatua watakazozichukua hazijawekwa wazi, huenda ikawa ni pamoja na kucheza ovyo katika michezo yao ijayo kwa lengo la kumfukuzisha kazi Mourinho.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*