googleAds

KOCHA ZAHERA ATIMUA WANNE YANGA KWA KUKOSA NIDHAMU

NA LULU RINGO


KOCHA wa klabu ya Yanga Sc Mwinyi Zahera amewasimamisha wachezaji wanne wa klabu hiyo akiwemo golikipa Ramadhani Kabwili, beki wa kushoto Haji Mwinyi na viungo Said Juma Makapu na Pius Buswita kutokana na utovu wa nidhamu.

Wachezaji hao walifanya utovu wa nidhamu baada kwa kutozingatia muda wa kufika mazoezini wakati wa maandalizi ya timu hiyo ilipokuwa ikijiandaa kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Stand United mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa siku ya Jumapili Septemba 16 ambapo iliibuka na ushindi wa bao4-3.

Zahera kupitia afisa habari wa timu hiyo, Dismas Ten amewaondoa wachezaji hao kambini na amewataka waendelee kutumikia adhabu hiyo hadi suala lao litakapo zungumzwa na uongozi wa klabu hiyo.

“Adhabu iliyotolewa na Kocha itaendelea hadi mchezo wa kesho utakapomalizika na baada ya hapo swala lao litarudishwa katika uongozi na kuona nini kinaweza kuamuliwa na uongozi kwa hatua za baadae” amesema Ten

Kesho Yanga itamenyana na Coastal Union ya Tanga mchezo huo umepangwa kupigwa usiku saa 1:00 katika uwanja wa taifa.

 

 

Previous Article

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*