TONTO DIKEH AKANA ‘KUBANJUA’ AMRI YA SITA NA MCHUNGAJI

LAGOS, Nigeria


BAADA ya kukaa kimya kwa muda mrefu kujibu shutuma zinazomkabili  kuhusu kuingia katika uhusiano wa kimapenzi na mchungaji, staa  mahiri katika tasnia ya filamu nchini Nigeria,  Tonto Dikeh, ameibuka na kukanusha madai hayo akisema ukimya wake alikuwa akitafuta  jinsi ya kijisafisha.

Hivi karibuni kimwana huyo alishutumiwa na vyombo vya habari na watu mbalimbali wakidai kuwa staa huyo ameingilia penzi la mwanamke mwenzake na kumpora mwanamume ambaye ni mchungaji  tajiri nchini Afrika Kusini, Shepherd Bushiri.

Hata hivyo juzi staa huyo alivunja ukimya na kuweka kila kitu hadharani, akiwa na rundo la risiti akisema kuwa fedha alizozipokea kutoka kwa tajiri huyo ilikuwa ni ada ya kuonekana katika mikanda ya kanisa  linaloendesha na mchunguaji huyo, jambo ambalo limeibua mwasili tena ni lini makanisa yakaanza kutoa hela ili watu mashuhuri waoanekna katika makani  yao.

“Tuhuma hizi nilikuwa nimezifahifadhi kwenye kitabu cha kumbkumbu zangu kwa sababu wiki hii nilikuwa na kazi nyingi za kijamii. Ndani ya wiki iliyopita nilikuwa nikishiriki katika kukusanya michango  katika matukio ya kijamii kama inavyofahamika hii ilikuwa ni wiki ya kupiga vita biashara ya kusafirisha binadamu na mimi ni balozi wake,”alisema staa huyo.

“Nisingependa kuyasema haya hadharani, lakini nimeamua kufanya hivyo kutokana na kuwa yameniumiza  na ukweli ni kwamba nilipigiwa simu na mmoja wa viongozi wa kanisa aliyejitambulisha kwa jina la  Brenda na wakaniomba nikaendeshe semina kwa ajili ya vijana na hivyo nikawafundisha vitu vingi likiwamo la familia yangu ambayo iliwagusa waumini wengi ambao wanasali katika kanisa hilo,”aliongeza staa huyo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*