ALI KIBA AFURAHIA KUMWOZA DADA YAKE

NA MWANDISHI WETU


MFALME wa Bongo Fleva, Ali Kiba, amemwoza dada yake, Zabibu Kiba, kwa mchezaji wa timu ya Taifa, Taifa Stars na Baroka FC ya Afrika Kusini, Abdi Banda, alfajiri jana katika Msikiti wa Sanene, Tabata, jijini Dar es Salaam.

Baada ya ndoa hiyo kufungwa hafla fupi iliyoambatana na kifungua kinywa ilifanyika katika nyumba ya Ali Kiba, huku ndugu wa karibu na familia ya msanii huyo wakipata nafasi ya kupiga picha za kumbukumbu.

Akizungumza jana, Ali Kiba alisema dada yake Zabibu ameingia katika nusu ya Dini ya Kiislamu na ndoa ni safari ambayo kila mtu ataipitia hivyo anamtakia kheri katika maisha hayo mapya.

“Kila kitu anapanga Mwenyenzi Mungu, imefikia ‘time’ yake ndiyo maana ameolewa, imekuwa baraka kwetu, mwanamke ndiyo kichwa katika familia, wawe na masikizano na aichunge ndoa yake,” alisema Kiba.

Hatua hiyo ya Zabibu kuolewa imekuja ikiwa miezi mitatu imepita toka kaka zake Ali Kiba na Abdu Kiba kuoa.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*