MASTAA HAWA HAWATAKWENDA URUSI

MOSCOW,Urusi


JANA ndiyo ilikuwa siku ya mwisho kwa makocha wa timu za  taifa kutangaza vikosi vyao vya  mwisho vitakavyokwenda kushiriki fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi huku ikishuhudiwa nyota kadhaa wakiachwa.

Kwa mujibu wa orodha ya vikosi hivyo, Kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps atakwenda katika michuano hiyo bila huduma ya nyota wake,  Laurent Koscielny, ambaye anakabiliwa na matatizo kifundo cha mguu  aliyokumbana nayo wakati wa mechi ya nusu fainali ya Ligi ya Europa kati ya  Arsenal  dhidi ya  Atletico Madrid.

Mbali na staa huyo pia  Karim Benzema naye takuwamo kutokana na staa huyo kufungiwa kuichezea timu hiyo na Dimitri Payet ambaye pia naye alipata majeraha ya misuli ya nyama za paja ambayo naye aliyapata wakati wa mechi ya fainali ya Ligi ya Europa.

Wakati Ufaransa ikiwa katika hali hiyo, Kocha wa  England, Gareth Southgate naye aliamua kuwatema nyota wawili wa Liverpool, Alex Oxlade-Chamberlain  na  Joe Gomez  kutokana na majeraha waliyoyapata mwishoni mwa msimu uliopita.

Nyota wengine  ambao watalazimika kuzishuhudia fainali hizo wakiwa nyumbani ni straika  wa Ubelgi, Christian Benteke, beki wa Brazil,  Dani Alves.

Mbali na hao pia kocha wa  Ujerumani, Joachim Low amemuengua nyota wa Manchester City, Leroy Sane licha ya msimu uliopita kuwa katika ubora wake.

Pia mbali na hao staa wa Inter,  Mauro Icardi naye hayumo kwenye kikosi hicho cha kocha Jorge Sampaoli kitakachoiwakilisha  Argentina na huku mlindamlango wa  Man Utd,  Sergio Romero naye akitemwa kutokana na kuwa majeruhi na huku .

Kwa wa Dermark aliyachwa ni staraika Nicklas Bendtner  naye akitemwa kwenye kikosi cha Denmark.

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*