OKWI AITWA KENYA

NA ALLY KAMWE, NAKURU


*Bocco naye ndani, ni baada ya Simba kutinga robo fainali SportPesa Super Cup

*Kiwango, penalti vyamponza Pierre Msimbazi

SIMBA imefanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano ya Sportpesa baada ya kuifunga Kariobangi FC ya hapa Kenya kwa penalti 3-2 na sasa itakutana na Kakamega FC katika hatua inayofuata.

Kwa kutambua umuhimu wa mchezo huo unaofuata, mabosi wa Wekundu wa Msimbazi wameamua kukiongezea nguvu kikosi chao kwa kuwaongeza mshambuliaji wao nyota, Emmanuel Okwi na John Bocco.

Okwi hakuondoka na kikosi hicho wiki iliyopita kwa kuwa alikuwa nchini Uganda kuitumikia timu yake ya Taifa ‘The Cranes’, wakati Bocco ni majeruhi.

Akizungumza na BINGWA Dar es Salaam jana, kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa Simba ambaye hakupenda jina lake kuandikwa gazetini, alisema wanatarajia kukiongezea nguvu kikosi chao kuelekea mechi za nusu fainali baada ya kubaini mapungufu kadhaa katika safu yao ya ushambuliaji katika mchezo wa jana.

Katika mchezo huo, washambuliaji wa Simba wakiongozwa na Mohamed Rashid aliyetua Msimbazi wiki iliyopita akitokea Prisons, walijaribu mara kadhaa kuipenya ngome ya Kariobangi bila mafanikio.

“Mfumo wa mwalimu ni mgumu, unawabana wachezaji. Hatukupiga mashuti golini, mwalimu hataki washambulie, anataka wacheze katikati. Mohammed Rashid muda wote yupo mbele kule, hajui la kufanya ukizingatia ni mchezo wake wa kwanza, akina Okwi na Bocco huwa wanashuka kuchukua mipira wenyewe na kupanda nayo kwenda kufunga.

“Tumeshinda kwa uzoefu, watu wameshakosa penalti mbili halafu mtu anafanya mchezo, anajua Tshabalala (Mohammed Hussein) kila siku anakosa penalti………………

Kwa habari kamili jipatie nakala ya gazeti la BINGWA hapo juu


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*