KICHAPO CHAMKERA KOCHA UJERUMANI

MUNICH, Ujerumani


KOCHA wa Ujerumani, Joachim Low, amesema amekasirika sana baada ya mabingwa hao kuendelea kuonesha kiwango kibovu ambacho juzi kilisababisha wafungwe na Austria.

Katika mchezo huo ambao ulipigwa mjini Klagenfurt, vijana hao wa Low ndio walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa nyota wao, Mesut Ozil, lakini baadaye wakajikuta wakilala  2-1 kutokana na mabao yaliyowekwa kimiani na mastaa Martin Hinteregger na Alessandro Schopf waliomtungua mlinda mlango aliyekuwa majeruhi, Manuel Neuer.

Mchezo huo wa kirafiki ulikuwa ni wa  tano kwa Ujerumani kuondoka uwanjani bila ushindi na huku wakiwa wamebaki na mmoja dhidi ya Saudi Arabia, kabla ya kufunga safari kwenda nchini Urusi.

Mtanange huo pia ulilazimika kuchelewa kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha na kisha ukamshangaza Low kutokana na kiwango kilichooneshwa na timu yake dhidi ya Austria, ambayo ushindi huo ulikuwa ni wa saba licha ya kushindwa kufuzu fainali za Kombe la Dunia.

“Nilishasema muda mfupi uliopita kuwa nimekasirika,” Low aliuambia mkutano wa waandishi wa habari.

“Sikukasirika kwa kufungwa, sikukasirika kupoteza mchezo, bali nimekasirika kwa namna tulivyopoteza,”  aliongeza kocha huyo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*