SALAMBA NASUBIRI MATOKEO YA KAMARI ULIYOCHEZA

 


HIKI ni kipindi cha dirisha kubwa la usajili. Kwa Ligi Kuu Tanzania Bara, kuna vita kali ya chini kwa chini kati ya klabu mbalimbali zinazosaka wachezaji wa kuviimarisha vikosi vyao.

Kama ilivyo kawaida, macho na masikio ya mashabiki wa kandanda nchini huelekezwa mitaa ya Kariakoo, kujua wachezaji waliosajiliwa na klabu zao za Simba na Yanga.

Hapo ndipo huibuka vijembe vya hapa na pale kati yao, kila upande ukijinasibu kuwa umenasa mchezaji/wachezaji wa kiwango cha juu.

Wakati mwingine, kwa kipindi hiki, ni kawaida kuwasikia mashabiki wa klabu hizo kongwe wakitambiana juu ya kiasi kikubwa cha fedha walichotumia katika usajili.

Ukiacha hayo, ni kawaida kila kinapofika kipindi hiki, kuona jina la mchezaji fulani likiwa gumzo sokoni na kuwaingiza vitani mabosi wa Simba na Yanga. Msimu uliopita, ilikuwa hivyo kwa Ibrahim Ajib na Haruna Niyonzima.

Safari hii, mbali ya wengine, kuna jina la Adam Salamba, mmoja kati ya mastraika wazawa waliokuwa tishio msimu uliomalizika siku chache zilizopita.

Akiwa na kikosi cha Lipuli FC ya Iringa, Salamba, alikuwa tegemeo la safu ya ushambuliaji ya timu hiyo, hasa baada ya Asante Kwasi kuondoka, ambaye licha ya ubora wake katika ulinzi, pia alikuwa mpachikaji mabao mzuri.

Kabla ya kumwaga wino kuwatumikia Wekundu wa Msimbazi, tayari kiwango chake kilimfanya kuingia katika rada za wababe wengine wa soka la Tanzania, Yanga na Azam.

Hata hivyo, binafsi bado nina shaka juu ya uamuzi wa Salamba kukubali ofa ya kwenda kujiunga na kikosi cha Simba, nikiufananisha na mtu aliyecheza kamari.

Si kwamba sijapenda Simba kufanikiwa kumnasa, ninachojiuliza ni hiki, Salamba amejiamini nini kwenda katika ushindani wa namba dhidi ya John Bocco na Emmanuel Okwi?……….

KWA HABARI ZAIDI JIPATIE NAKALA YAKO YA GAZETI LA BINGWA HAPO JUU

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*