ROONEY AZIFUATA SH BIL 22

WASHINGTON, Marekani


 

JUZI kamera za waandishi wa habari zilimnasa staa, Wayne Rooney, akitua Marekani ikiwa ni mpango wake wa kwenda kumalizana na mabosi wa DC United.

Taarifa za awali zimedai kuwa Mwingereza huyo atalipwa mshahara wa pauni 7.5 (zaidi ya Sh bil 22 za Tanzania) kwa mwaka na hiyo ni nje ya posho.

Rooney mwenye umri wa miaka 32, ameshakuwa na mazungumzo ya awali na timu hiyo licha ya kuwa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake wa sasa wa Everton.

Alijiunga na Everton Julai, mwaka jana, klabu aliyojiunga nayo akitokea Manchester United aliyokuwa ameitumikia kwa misimu 13.

Mshambuliaji huyo alikuwa mchezaji muhimu Everton katika msimu uliokwisha, akicheza mechi 40 na kufunga mabao 11.

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*