MDOGO WAKE HAZARD ATIMULIWA BLUES

LONDON, England

ALIYEWAHI kuwa Kocha Msaidizi wa Chelsea, Ray Wilkins, amekosoa usajili uliofanywa na timu hiyo wa kumchukua Kylian Hazard, ambaye ni mdogo wa winga machachari wa timu hiyo, Heden Hazard.

Kylian alitua Blues juzi baada ya kukamilisha usajili wake akitokea katika klabu ya Ujpest ya nchini Hungary.

Chelsea wameuza chipukizi wengi na wengine wakiwatoa kwa mkopo, jambo ambalo limemfanya Wilkins kuamini Kylian hakuwa na nafasi yoyote kwenye kikosi cha Chelsea.

“Chelsea wana makinda wengi wenye uwezo wa ajabu,” alisema Wilkins alipokuwa akihojiwa na mtandao wa talkSPORT. Kwa kweli sijaona sababu ya kufanya hivyo (kumsajili Kylian).”

Kylian mwenye umri wa miaka 22, amesajiliwa na Cheslea baada ya kuichezea Ujpest mechi 42.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*