15 KUWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA VPL

Lulu Ringo, Dar es Salaam        |        


Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), hii imeteua wachezaji 15, kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa mwaka 2017/18.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kamati hiyo, wachezaji hao ni miongoni mwa wachezaji 30 waliotangazwa wiki mbili zilizopita kuwania tuzo hizo, ambapo watachujwa kulingana na takwimu mbalimbali za ligi hiyo na kubakia watatu.

Taarifa hiyo imesema majina ya wachezaji hao watatu yanatarajiwa kutangazwa wiki ijayo, ikihusisha upigaji kura kutoka kwa wahariri wa habari za michezo, manahodha wa timu za Ligi Kuu na makocha wa timu za Ligi Kuu.

“Wachezaji hao na majina ya timu zao kwenye mabano ni Obrey Chirwa, Papy Tshishimbi na Kelvin Yondani (Yanga),  Shafiq Batambuze, Mudathir Yahya naTafadzwa Kutinyu (Singida United).

“Wengine ni Adam Salamba (Lipuli), Habibu Kyombo (Mbao), John Bocco, Emmanuel Okwi, Shiza Kichuya na Erasto Nyoni (Simba), Marcel Kaheza (Majimaji), Yahya Zayd (Azam) na Hassan Dilunga (Mtibwa),” imesema taarifa hiyo.

Licha ya Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL, zilizopangwa kufanyika Juni 23, mwaka huu katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam zitatolewa tuzo mbalimbali ikiwemo ya Bingwa wa VPL, mshindi wa pili, hadi wa nne na mfungaji bora.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*