googleAds

Zahera awatibua mashabiki Yanga

ZNA MWAMVITA MTANDA

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amezua balaa kwa mashabiki wa timu hiyo baada ya kikosi hicho kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Lipuli FC.

Mchezo huo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara ulichezwa juzi katika Uwanja wa Samora, Iringa.

Akizungumz na BINGWA jana, sJuma Kibiki ambaye ni shabiki mkubwa wa  Yanga kutoka tawi la kitunda, alisema  kitendo cha kocha huyo kuondoka kimesababisha timu yao kufungwa.

“Zahera ameanza kutuvuruga kwanini aondoke kabla ya mechi, alikuwa anawahi kitu gani wakati kocha mkuu wa timu ya taifa ya DR Congo alikuwa hapa, au anataka tuukose ubingwa, ukweli ninamlaumu sana.

“Naamini kabisa kama angekuwepo tusingefungwa na Lipuli maana mbinu anazijua ila anataka kuvuruga mambo mwenyewe, sisi tunamkubali lakini awe makini, watu wanataka ushindi katika kila mchezo wa Ligi Kuu,” alisema Kibiki.

Aidha, Kibiki aliongoza kuwa kama Yanga itaendelea kupata matokeo ya aina hiyo ubingwa watabaki kuusikia tu.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*