Tanzania yazidi kung’ara tenisi A/Mashariki

NA GLORY MLAY

WACHEZAJI wa Tanzania wameendelea kutamba katika mashindano ya tenisi Afrika Mashariki na Kati ‘Tennis Zone Championship’, yanayofanyika kwenye Uwanja wa Gymkhana, Dar es Salaam.

Katika mchezo wa kwanza, Kanuti Omari wa Tanzania aliibuka kidedea baada ya kumfunga, Salum Mutabazi, kutoka nchini Burundi kwa pointi 12-3, ambapo mzunguko wa kwanza alishinda seti 6-1 na raundi ya pili seti 6-2.

Ismail Rashidi naye kutoka Tanzania alishinda pointi 12-3 dhidi ya Catoto Kim wa Burundi, akishinda seti 6-1, 6-3 katika mizunguko yote.

Naye John Godfrey wa Tanzania, alimchapa, Mohamed Said kutoka Comoro kwa pointi 12-3, ambapo mzunguko wa kwanza alishinda seti 6-1 na uliofuata 6-2.

Katika mchezo mwingine, Joseph Cyiza kutoka Rwanda, alifanikiwa kumfunga Sagati Ismail wa Kenya pointi 12-7, akifunga seti 6-0, wa pili alifungwa seti 6-3, lakini akafunga seti 6-4 mzunguko wa mwisho.

Naye Faith Urasa wa Kenya, aliibuka kidedea baada ya kumfunga Mtanzania, Barnaba Molel, pointi 12-3, akishinda seti 6-0, 6-3.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*