Sterling amwagiwa sifa kibao

MANCHESTER, England

WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, amepewa sifa kibao na mchambuzi wa kituo cha Sky Sports, Ian Wright, baada ya mchezaji huyo kufunga mabao mawili dhidi ya Crystal Palace.

Timu hiyo inayonolewa na Pep Guardiola, walishinda mabao 3-1 huku Gabriel Jesus akifunga bao jingine kati ya hayo, lakini Sterling alionekana kumfurahisha zaidi mchambuzi huyo.

“Kila siku anakuwa mpya mbele ya lango la wapinzani, anatulia na kufanya maamuzi mazuri, amebadilika sana shukrani ziende kwa Guardiola sababu amembadilisha sana,” alisema Wright aliyewahi kucheza Arsenal.

Mechi ijayo Manchester City watakutana na Tottenham mfululizo katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na Ligi Kuu ya England.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*