Solskjaer: Hao Chelsea tutawashangaza kwao

MANCHESTER, England

OLE Gunnar Solskjaer ana hasira huyo. Kuelekea mechi ya Kombe la FA kati ya Chelsea na Man Utd itakayochezwa usiku wa leo, kocha huyo wa mashetani wekundu amepania kuondoka Stamford Bridge na ushindi.

Solskjaer alisema kuwa anatarajia kuishuhudia timu yake hiyo ikiibuka na ushindi ingawa alikiri hautopatikana kwa njia nyepesi na huenda historia ikajirudia leo.

Man Utd itacheza na Chelsea katika mchezo wa raundi ya tano Kombe la FA, baada ya kuing’oa Arsenal katika raundi iliyopita na Solskjaer anasubiri kuona historia ya mwaka 1999 itakavyojirudia.

“Nakumbuka mwaka 1999 tuliifunga Chelsea kwenye uwanja wao wa nyumbani, tukaibuka na ushindi dhidi ya Arsenal na Liverpool na kutangazwa mabingwa wa FA.

“Tulipata upinzani mkali na ndicho ninachokiona msimu huu. Kama tunahitaji kucheza fainali hatuna budi kupambana,” alisema kocha huyo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*