Salah: Bado mechi nne tuwe mabingwa

MERSEYSIDE, England

WINGA wa Liverpool, Mohamed Salah, anaamini kuwa timu yake wakishinda michezo minne iliyobaki, wanaweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England msimu huu licha ya kupata ushindani mkubwa kutoka kwa Manchester City.

Salah alifunga bao la pili katika mchezo wao wa juzi dhidi ya Chelsea kwa shuti kali na kufanya mbio za ubingwa wa ligi hiyo kuwa ngumu zaidi kwa Manchester City waliobaki na michezo mitano.

“Naamini tutashinda michezo iliyobaki na kuombea Manchester City wapoteze, naamini tutakuwa mabingwa msimu huu,” alisema Salah.

Liverpool wamebakiwa na michezo dhidi ya Cardiff City, Huddersfield, Newcastle United na Wolverhampton.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*