Nandy, Jux, Harmonize wazindua Coke Studio Africa

NA CHRISTOPHER MSEKENA

MSIMU mpya wa Coke Studio Africa umezinduliwa kwa mafanikio makubwa jijini Dar es Salaam, kwa mastaa wa Bongo Fleva, Nandy, Jux, Harmonize na Rayvanny kuwapa burudani mashabiki.

Akizungumza na Papaso la Burudani katika uzinduzi huo uliofanyika juzi Life Club, Mwenge, Nandy alisema kupata nafasi ya kufanya kazi na Skales wa Nigeria ni jambo kubwa kwenye muziki wake.

“Ni mtu ambaye nilikuwa namwona kwenye TV na mimi ni shabiki yake mkubwa, hivyo kufanya naye kazi sikutegemea kama ni mtu ambaye yupo poa kiasi kile,” alisema Nandy.

Katika msimu huu mpya wa Coke Studio, Jux atashirikiana na mrembo Shellsy Baronet wa Mozambique, Harmonize atashirikiana na staa wa Uganda, Sheebah Karungi huku Rayvanny akitengeneza kolabo na Naiboi wa Kenya huku kwa mara ya kwanza mashabiki watamwona Mimi Mars.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*