Minziro: Naiandalia Simba dozi ya kushtua

WINFRIDA MTOI

KOCHA Mkuu wa Singida United, Fred Minziro, amesema kuna uwezekano wa kukutana na Simba ikiwa imeshatangaza ubingwa, hivyo atawaandalia dozi itakayowashtua.

Singida United juzi ilitoka sare ya mabao 2-2 na JKT Tanzania kwenye Uwanja wa Namfua, Singida, mechi inayofuata watakutana na Simba, Mei 21 katika dimba hilo.

Akizungumza na BINGWA jana, Minziro, alisema baada ya kutoka sare ya JKT Tanzania, presha ya kuhofia kushuka daraja imezidi kupanda.

Alisema ili presha yake itulie, mchezo wa Simba anahitaji kupata pointi, hali  inayomfanya kutumia muda uliobaki kuandaa kikosi chake kama wanacheza fainali.

“Simba ni timu bora hakuna ubishi na inawezekana tukakutana nayo ikiwa imeshatangaza ubingwa, ila watakachokutana nacho huku watashangaa,” alisema.

Minziro alisema mechi hiyo ndiyo itakuwa ya mwisho kucheza katika uwanja wao wa nyumbani na anataka kuweka heshima kama alivyopandisha kikosi hicho.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*