Lipuli wapangua kikosi

NA WINFRIDA MTOI

KOCHA Mkuu wa Lipuli FC, Samweli Moja, amesema katika mchezo wao dhidi ya Yanga, kikosi chake kinatarajia kuwa na mabadiliko tofauti na kile kilichokutana na Simba na kufungwa mabao 3-1.

Lipuli itakutana na Yanga kesho katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaopigwa kwenye Uwanja wa Samora, mkoani Iringa.

Akizungumza na BINGWA, Moja, alisema walipokutana na Simba, waliwakosa washambuliaji wao wawili ambao ni Miraj Athuman aliyepata msiba wa kaka yake na Zawadi Mauya aliyekuwa majeruhi.

Alisema wachezaji wote hao tayari wamerejea kikosini na Mauya alianza kuonekana katika mchezo uliopita dhidi ya Mbao uliopigwa Samora, wiki iliyopita na kutoka suluhu.

“Nimewaangalia wachezaji wote katika mazoezi wanaonekana wako fiti, lazima waniongezee nguvu katika safu ya ushambuliaji kwa sababu tunachohitaji ni kutumia nafasi tutakazopata  kufunga mabao,” alisema Moja.

Katika msimamo wa ligi hiyo, Lipuli ipo nafasi ya tano na pointi 39, ikicheza mechi 30, ikishinda tisa, sare 12 na kupoteza tisa, wakati Yanga inaongoza ikiwa na pointi 67 ilizozipata kwa michezo 27.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*